Conficker mnyoo hatari aprili mosi
Aprili mosi inasadikiwa tarakishi zipatazo milioni 12 duniani kote zitaathirika kwa mnyoo uitwao Conficker .Kinachoogopesha zaidi ni kwamba kimnyoo hiki haijulikani hasa ni kitu gani kitafanya.Tarakishi iliyoathirika itatengeneza kile kinachoadikiwa tarakishi yenye uwezo mkubwa katika kufanya lolote baya kwenye tarakishi za watu bila kipingamizi chochote.Tayari kampuni ya Microsoft wametoa bakshishi ya $ 250000 kwa yeyote atakaetoa taarifa na kukamatwa wahusika waliondika programu hii.Ni muhimu kujua jinsi ya kuweza kujikinga na mnyoo huu ambao moja ya madhara yake makubwa unafuta kazi zako na kuharibu mfumo mzima wa muingiliano,bonyeza hapa usome maelezo zaidi na jinsia ya kujikinga.




4 Comments:
Inaonekana huu mnyoo ni hatari sana. Nilitazama kipindi katika CNN walikuwa wanawahoji wataalamu wa usalama wa kompyuta na hakuna aliyekuwa na uhakika wa jinsi ya kuuzuia. Ndiyo maana Microsoft wametoa zawadi wa dola 25,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa jamaa walioufyatua. Ngoja tuone hiyo April 1 itakuwaje!
Inaonekana huu mnyoo ni hatari sana. Nilitazama kipindi katika CNN walikuwa wanawahoji wataalamu wa usalama wa kompyuta na hakuna aliyekuwa na uhakika wa jinsi ya kuuzuia. Ndiyo maana Microsoft wametoa zawadi ya dola 250,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa jamaa walioufyatua. Ngoja tuone hiyo April 1 itakuwaje!
Wenyewe wameshindwa,ninachofahamu huwa wanapotangaza dau hadharani la kukabiliana na hawa wanaoitwa "hackers" ina maana walishapambana vita ya kimya kimya waka salenda.
Atakaezuia basi ndio huyo huyo mtengenezaji.
gonikikwambia nimimi hutasadiki, basi kama unataka hizo madola niriport! mambo vipi mkuu mbona kimya sana kunani kitabu kimekukunjia nini?
nilitegemea ungedokeza madhara ya kinyoo hiki ilipotimu april 1. au ndo kujisahau?
pamojah!
Post a Comment
Links to this post:
Create a Link
<< Home