Sakata la Miss tz na ubaguzi wa rangi
Juzi jumamosi huku mawazo yangu yakiwa katika gemu ya Jk boys na timu ya taifa ya Uganda,ndio nikashtuka kuwa yale mashindano ya kumsaka kisura wa tanzania ya kila mwaka nayo yanafanyika usiku huo.Katika gemu ya Jk boys iliisha kama nilivyotarajia kwa washakaji kushinda. Lazima nikiri wazi kuwa tangu warembo wetu hao wakiwa kambini kwa kujiandaa na mtanange huo sikuwa nawafatilia kwa ukaribu sana
Kwanza niwape ya mitaa hii
Mtanange kama huo ulishafanyika hapa.Mashindano haya hapa ni ya pili kwa kuwa na umaarufu baada ya kriketi.Kila kona ndio gumzo.Wadada wa hapa ndio sehemu yao ya kutokea.Mashindano haya mitaa hii yameleta wadada poa sana yaani kila wakati wakionyeshwa kwenye television hutatamani waondoe picha zao.
Mfano angalia mrembo kama Aishwarya Rai(Miss India 94 baadae akaja kuwa miss dunia 1994)Leo Rai ni mmoja wa masupastaa wa Bollywood.Kifaa kingine adimu ni Priyaka Chopra(Miss India 2000 na baadae Miss dunia 2000).Ebwanaee kuna hiki basi tu, kifaa adimu kama Neha Dhupia(Miss India 2002) sio cha kubeza .Vifaa vipo kibao mitaa hii kungine ni hiki Yukta Mookhey(Miss India 1999 baadae Miss Dunia).Niishie hapa kwa kuwataja hao wachache Nilipoona Miss Kinondoni 2007 ana asili ya udosini nikajua kutakuwa hakukaliki jijini Mzizima watu weeewee watu ahaaa! Si mchezo.Maoni niliyoyasoma Bongocelebrity yalinistua sana lakini nikapuuzia tu nikajua sidhani kama watanzania tunaweza kufika umbali mrefu huo wa kuhoji rangi ya mrembo wetu,kwa kujua kuwa watanzania hatuwezi kuvumilia dhambi hii kubwa ya ubaguzi.
Niwape hii
Ijumaa nilikwenda kwenye onyesho la jamaa fulani anaitwa Steven Kapur au kwa jina lingine kama Apache India.Jamaa huyu ni mdosi full ila alizaliwa Uingereza, anapiga mitindo ya rege na Bhangramuffin(mchanganyiko wa dancehall na Bhangra) jamaa ukimsikiliza huboreki kamwe.Jamaa masongi yake yana ujumbe sana.Alikuwa anatoa store kwa washikaji baada ya onyesho.Alisema haya:
- “…rascim is still rampat and is not atrivial issue anybody who has actually not seen it can cannnot comment on it….”
kwa kauli ile tu nilipata marafiki kibao pale wakawa washikaji zangu. Kauli hii kumbe alikuwa anaota itatokea kesho yake bongo.
Miss tanzania 2007 ni Richa Adhia.
Alifaa au hakufaa?Majaji ndio waamuzi wa mwisho.Tatizo sasa limezuka suala la ubaguzi unaofanywa na watanzania wachache dhidi ya mrembo huyu.Kisa ana rangi nyeupe si ana asili toka udosini!.Hii kitu kweli mimi inanisikitisha sana dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana alisema Mwalimu nyerere,ukianza ni sawa ni kula nyama ya binadamu mwenzio.Hii watanzania tumefika mbali sana.Usiku ule nilipata SMS kama 3 hivi toka Bongo zikikejeli ushindi wa mrembo Richa.Moja ilinitia simanzi sana jamaa kakandamiza sana na kusema: "…miss India anaeishi Tanzania…”
Kauli hizi ndio zinatawala sana kwa sasa.Napinga ubaguzi wa rangi maana najua machungu ya kubaguliwa kama alivyosema Apache,mwanzoni wakati wa vuguvugu za Afrika kusini akina Steve Biko sikuwalewa vizuri walipokuwa wakipinga kwa nguvu ubaguzi na sikujua machungu ya kubaguliwa kwa rangi yako.Unaweza kuingia kwenye treni watu wakainuka kwenye siti woote kisa hawataki kukaa na kaluu.Noma sana hii.
Sasa hii imeanza na nyumbani.Tunaanza kubaguana sisi kwa sisi na itaota mizizi na kuanza kubaguana ndugu kwa ndugu kisa mie mweusi kaka yangu mweupe.Tunajenga jamii gani watanzania wenzangu? Dunia hii tambarale sio duara tena kuna muingiliano mkubwa wa kijamii.Kuwa mtanzania lazima uwe mweusi? Wengine wanahoji kazaliwa wapi.Kuna watu wengi wamezaliwa nje ya tanzania na wanafanya mambo mema kwa nchi yao.Kuzaliwa nje ya nchi sio kigezo cha kumbagua mwenzako.
Lakini mbona tuna wabunge wenye asili ya udosini na arabuni? Wale vipi au ndio kusema watanzania wameanza kutoa boriti ya mrembo Richa kwanza na watakuja kwa waheshimiwa hao?.Sijui. Ili kuweka sawa muingiliano wa kijamii baada ya ushindi ule niliwaonyesha mabinti wa hapa kuwa tuna mrembo mwenye asili kama yao.
Kweli walifurahi sana.Na wakaona kuwa inawezekana hata wao kuingia moja kwa moja katika jamii yetu.Tatizo lilikuja wakataka niwatafsirie oni moja baada ya lingine katika blogu ya michuzi katika picha ya mrembo Richa.Wakasema inaonekana anakubalika sana.Maoni mengine ikabisi nianze kudanganya maana ingefanya watuelewe ndivyo sivyo jamii yetu.Jamii ambayo iko katika kizazi cha dijitali. Watanzania wenzangu tunaandaa kizazi gani cha dijitali na ubaguzi wa sisi kwa sisi?
Picha na Bongocelebrity na Google




2 Comments:
Kuna marekebisho kidogo hapo katika mtundiko. Taifa Stars walicheza na Cranes ya Uganda, sio na Msumbiji.
Pole kwa kitabu kijana wetu.
Naomba niungane na wewe kulaani tabia hii ya ubaguzi, kwa kweli sikutarajia kama Wabongo tumefikia hatua ile, inasikitisha sana. Nilisoma maoni ya wachangiaji katika blogu ya Michuzi kuhusu maamuzi ya majaji wa shindano lile, yaani utachoka.
Sielewi kwa nini sisi tulalamike kubaguliwa tukiwa nje ya nchi wakati na sisi tunafanya hayo hayo.
Ahsante kaka nimeufanyia marekebisho mtundiko huu.
Inasikitisha sana kweli na sijui tunaelekea wapi na ubaguzi huu?
Post a Comment
Links to this post:
Create a Link
<< Home