Kama unapenda Utamaduni kwanini unavaa Nguo?
Picha kwa hisani ya Mrocky .Mamiss Kinondoni wakitoa zawadi kwa watoto yatima.Makala yenyewe aliandika Ndesanjo Bonyeza hapa.Mule ndani kuna mistari poa sana inanifanya nirudie rudie kusoma makala hii.Suala hili ni gumu kueleweka kuna wengine wanafanya vitu wanaonekana kinyume katika jamii yetu.
....Kama unapenda utamaduni wa Mwafrika kwanini unavaa nguo? Kwanini unavaa viatu?.... Utamaduni ni neno pana sana Ikaendelea tena baadhi ya mstari...hawajui historia yao maana asingekushangaa wewe kama Mwafrika kuvaa nguo na kutetea utamaduni wako . Hajui kuwa viwanda vya mwanzo kabisa duniani vya nguo vilikuwa vipo katika bara lake?.....Lakini hivi vivazi vya sasa kiboko! sijui ni utamaduni wetu?
Kuna mstari mwingine unasema .....Akikwambia kuwa Wamasai wanafuata utamaduni, ili kumsumbua tu akili, muulize, “Mbona Wamasai wanavaa viatu vya matairi? Kwani matairi ni sehemu ya utamaduni wa Kimasai? Matairi ya magari wamerithi toka kwa mababu zao? Kwani mababu zao walikuwa wana magari? Matairi kama General Tyre na Firestone si yametoka kwa watu weupe?”.....Hii labda tusilaumu sana vivazi vya kileo wakifikiri kuhusu kufata utamaduni wao wanaogopa kuvaa viatu vya matairi!
Alafu hapa ndio tatizo....ninaposema utamaduni ninamaanisha tu ukale. Ndio, ninamaanisha ukale, ila hiyo ni sehemu ndogo ya utamaduni. Sio mwanzo na mwisho. Ninamaanisha ukale. Ninamaanisha pia na “usasa” maana jamii yetu sio jamii iliyosimama kama mti wa mbuyu. Kama zilivyo jamii nyingine duniani, ni jamii inayobadilika na kukua...




6 Comments:
Mzee hapa umegusa,nitakujibu,ngoja kwanza.
Karibu rasta.
Duh!
Samahani! Egdio !Vipi mafuriko hapo kwako, hayakukufikia?
Simon sijafikiwa na mafuriko niko mbali sana na kule.Hilo balaa limepita pembeni
ARE YOU AWAKE MR PRESIDENT?
Hebu rejesha nyuma fikra zako mpaka mwezi Januari mwaka 2006, muda mfupi baada ya rais mpya Jakaya Kikwete kuapishwa kushika usukani wa Tanzania Company Ltd [Jamhuri ya Muungano wa Tanzania].
Idadi kubwa ya watanzania, naweza kudiriki kusema takriban asilimia 75 walikuwa na ndoto,...ndoto ya kuona maisha yao yakibadilika na kuwa bora.Si wamepata rais aliyeteuliwa na Mungu kuja kuwaokoa?[God's chosen president].
Sasa basi.....peleka mbele fikra zako mpaka wakati uliopo, kwa faida ya mjadala tuseme August 2007; rais Kikwete na serikali yake wamepoteza mwelekeo, kama ni mlevi tunasema kaanguka "chali".Ahadi walizotoa wameshindwa kuzitekeleza, wameshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo yaliyojitokeza na wamezidi kuahidi mengine chungu tele wakiwa hawajui maswala ya kuyapa kipaumbele [priority issues].Wanashika hili wanaachia kisha wanagusa jingine na kudakia kila wanalokosolewa.
Hivi mnaamini kwamba kimaendeleo tunaachwa na nchi zilizokuwa vitani kama Uganda na Rwanda?Aibu gani hii kwetu, what are we good at?Tuna madini [almasi, dhahabu, tanzanite, iron etc] tuna gesi [Songas and Artumas ni ushahidi bila kugusia mafuta ambayo mnajikanyaga kuhusu jinsi ya kuchimba], tuna bahari na maziwa na tuna mbuga za wanyama, lakini pia tuna ardhi kubwa yenye rutuba.Na juu ya yote hayo, tuna wananchi watiifu, ambao kama tungewashirikisha katika miradi ya maendeleo na kuwalipa haki yao ipasavyo, hakika Tanzania tungekuwa mbali.
Hata hivyo, japokuwa watanzania wana sifa ya kusahau haraka ahadi hewa kuliko binadamu wengine barani Afrika, kuna wasi wasi kwamba wakati huu chama tawala [CCM] kikashangazwa na nguvu ya kura [protest vote] kutokana na kupoteza imani na dhamana waliyopewa na wananchi.
GREED
Jaribu kufikiria, maisha lavish wanayoishi wabunge.Mishahara ni unyonyaji mkubwa - inakuwaje boss wa TRA alipwe milioni sita [6,000,000 plus] kwa mwezi mmoja, halafu mwuguzi alipwe chini ya 100,000 kwa mwezi?Hapa ndipo patamtoa jasho mwanajeshi mstaafu.
Na sasa wafanyakazi wanaandamana wakipigania haki yao ya kimsingi; hivi kweli rais na baraza lake la mawaziri pamoja na wabunge wanalala usingizi mzuri? Nauliza hivyo kwasababu nataka kujua endapo wana chembe chembe zozote za uchungu wa kuwakwamua watanzania wenzao.
POVERTY
Kwa kawaida mwezi una wastani wa siku 30, kima cha chini cha mtumishi wa sekta ya umma ni shilingi 78,000 - kwetu sisi tusiofahamu vyema hesabu ukigawa hicho kipato kwa 30 unapata jibu la shilingi 2600 kwa siku.
Mathalan, mtumishi anayepata huo mshahara anaishi nyumba ya kupanga [15,000 kwa mwezi], ana watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18.Anaishi Mbagala, kibarua anafanya maeneo ya Magogoni kama mlinzi wa ofisi ya wizara ya mambo ya nje - nauli kwa siku 1000.
Mpaka hapo sijaweka hesabu za chakula na matibabu.Sijajumlisha mambo ya ada ya shule kwa watoto.Huyu mtumishi anatoa wapi hiyo fedha nyingine inayohitajika aishi kwa uhakika wa kujua kesho atakula nini yeye na familia yake?
Jamani mbona hatuoneani huruma?Siamini kabisa viongozi wetu wana ubinadamu, ukweli ni kwamba wamebadilika na kuwa madubwana [monsters] wamejawa na unafiki, uchoyo na roho mbaya.
ARROGANCE
Kibaya zaidi ni kwamba nahodha Kikwete anachekelea japokuwa anaona jahazi likizama chini ya usimamizi wake, kuna mageuzi yanaendelea chini chini ambayo mwisho wake utakuja kuwa historia kubwa kwa CCM na siasa za Tanzania.
Fikiria serikali inaulizwa kuhusu matumizi ya sarafu ya dola, waziri husika anasimama na kukanusha kwamba: "hilo siyo tatizo; hakuna kitu kama hicho, shilingi bado ndiyo sarafu rasmi ya Tanzania,"
TRIVIAL
Naye waziri mkuu badala ya kukiri na kuahidi kuchukua hatua kurekebisha, anasema "serikali itatoa tamko".Hayo matamko hayatufikishi popote,DONT TRVIALISE MATTERS OF NATIONAL SECURITY, MATTERS OF NATIONAL INTEREST....tukuulize kwani benki kuu kazi yake nini?Ina maana wao au wewe hujui hilo MR EL?
Hatujasau malumbano ya posho ya wanafunzi, ingawa nasikia chuo kikuu kipya [Chimwaga University] kitakuwa na wanafunzi 20,000, kama ni 3000 kashese, basi wakiwa 23,000 litakuwa JISHESHE!
Kuna pia swala la marekebisho ya katiba, kuna swala la mikataba ya madini, kuna maafisa wa serikali wanaojulikana kufanya ubadhirifu wa fedha za umma [Richmond]......Bank of Tanzania maafisa wamesema hawajiuzulu [lakini ulisikia wapi mtanzania akajiuzulu ulaji?] anyway, orodha ni ndefu.
Hivi...mheshimiwa rais...unataka kutueleza sisi watanzania [waajiri wako] kwamba maafisa wako wote waandamizi ni wasafi?Kwa maana kwamba tangu uingie madarakani haujawahi kubahatika kumpata afisa hata mmoja aliyefanya uhalifu.Una bahati kweli kuzungukwa na watu wasafi....kila la heri, historia itakukumbuka sana kwa mema unayowafanyia watanzania.....Ndiyo, maisha bora kwa kila mtanzania.
WAKE UP!
Support uliyokuwa nayo ni kubwa, ni vyema kusema haujaipoteza yote.Bado una nafasi, nafasi ya kurekebisha.Vinginevyo historia itakuadhibu, it's time to do something; WALK THE TALK, action with big strides.SEE YOU AROUND MR PRESIDENT.
Post a Comment
Links to this post:
Create a Link
<< Home