Vitu vinane usivyojua kuhusu mimi.

Nimefuma picha hio hapo juu ya mzee wangu akiwa na mzee wake enzi zile.Simon kuna kazi hapa.Kuna vitu ambavyo havijulikani kuhusu mimi.Lakini hivi ni nane tu:
1.Napenda kuimba lakini sina sauti nzuri.
2.Napenda sana wasichana weupe
2.Napenda sana wasichana weupe
3.Sipendi kuosha vyombo.
4.Sili nyama nyekundu wala maziwa.
5.Sijawahi na wala sipendi kuhudhulia mahafali yangu.
6.sipendi usingizi
7.Kuna siku nilimtwanga jirani yetu jiwe la jichoni,nilipata kipigo sitasahau nilichangiwa na mama,baba,dada na kaka wawili nilikimbia nikalala nje ya nyumba.
8.Napenda ku date na wasichana wa mtandaoni.
5.Sijawahi na wala sipendi kuhudhulia mahafali yangu.
6.sipendi usingizi
7.Kuna siku nilimtwanga jirani yetu jiwe la jichoni,nilipata kipigo sitasahau nilichangiwa na mama,baba,dada na kaka wawili nilikimbia nikalala nje ya nyumba.
8.Napenda ku date na wasichana wa mtandaoni.
Na hawa naomba watuambie vitu vinane tusiojua kuhusu wao
1.Shamim
3.Mwandani
7.Mwaipopo
8.Ndabuli.





6 Comments:
Kumbe tusiopenda kunywa maziwa tuko wengi. Eti halafu tulikuwa tunafuga ng'ombe na babu ni mfugaji.
Najaribu kuimajini ulivyotoka baruti baadaya kumpiga jiwe jirani LoL
maziwa mimi mwenyewe sipendi lakini kwasasa najifunza kuyanywa kwaajili ya matatizo ya tumbo, lakini egidio nyama kwanini upendi? inakudhuru ukila? umeshawahi kuila? jaribu mbuzi choma au kmoto mwana hautaacha, utaniambia mwana!
Mmejaribu maziwa ya soya? Au ya mchele? Jaribuni tena yaliyochanganywa na vanilla. Mtaniambia.
Egidio, umenikumbusha nami enzi zangu za kulala nje. Ilikuwa mbinu ya kukwepa kuchapwa.
Mabinti wa kihindi unawapenda? Sema ukweli:)
@Ndesanjo: Maziwa ya soya na mchele mimi siyaiti maziwa.Nahisi ni ukosefu wa jina jipya kuyaita maziwa.Hayo mimi nayanywa siku moja moja.
Mimi najua kuwa maziwa ni yale yatokanayo an wanyama tu,au? hayo ya soya na mchele hata mimi nayanywa.Kama alivyosema Simon sijui kama ni sawa kuyaita maziwa!
Ndesanjo kwa swali lako nina kugugumizi kwa sasa.
Umenisikitisha sana kuhhusu swala la kutopenda Mahafali na kutohudhuria. Nami pia sipendi lakini nafikiri ni muhimu kuhudhuria kwa ajili ya familia yako, kwa ajili ya watoto wako, kwa ajili ya wajukuu zako - wape kumbu kumbu.
Zamani nilikuwa sipigi picha, nimeenda jeshini sikupiga picha eti kwa sababu mie "mgumu" Picha chache nilizotokea kuwemo kwa bahati mbaya wakati nikiwa jeshini na rafiki zangu kuwa nazo ndio izo zionapendwa ajabu na watoto wangu.
Kumbuka wakati mwingine tunalazimika kufanya vitu sio kwa sabu tunavipenda ila kwa sababu inabidi tuvifanya kwa faida ya watu wangine.
Je unakumbuka Mwalimu Nyerere alikataa kutoa interview kwa ajili ya kitabu? je angetoa si ingekuwa faida sana. yeye alikataa kwa kisingizio eti kila kitu anachokijua yeye kipo tayari outthere ni kazi ya waandishi kutafuta kiko wapi na kuandika na kwamba hana zaidi. Nafikiri kama angegranti interview sisi ndio tungefaidika zaidi kuliko yeye lakin ialiamua kutunyima uhondo huo!
Post a Comment
Links to this post:
Create a Link
<< Home