Saturday, July 21, 2007

Udereva mzuri kwenye kona!

Udereva wa nchi hii unasifika sana lakini mimi kwenye hii kona kwenye picha hapo chini mtaa ninaoshi mimi, huwa na mashaka sana kila siku.Huwa nawaza sana kama gari likishindwa kukata kona hio itakuwaje.Sasa jana mida ya saa mbili asubuhi(mida hio huku sio mida ya kazi kazi wanaanza saa nne baada ya kula chapati na kalamati zao) mama mmoja mke wa kibosile akiwahi kuwapeleka wanawe shule alifanya kile ambacho nimekuwa nikiwaza siku nyingi kuhusu hii kona.

Yule mama alilivaa geti kuu(picha ya chini) na kuingia ndani na kuparamia mlango mkubwa mweupe katika picha ya juu na kuvunja vunja mlango na kuharibu gari lililokuwa limeegeshwa ndani.Mimi wa juu kidogo hapo nilikuwa salama.lakini hakuna alieumia woote walikuwa wamefunga mikanda ya tahadhari.
Nilishindwa kupata picha za tukio sababu polisi walijaa kwa haraka sana kutokana na unyeti wa mtaa huu.Nilipoonwa na kamera yangu ikachukuliwa kwa muda nikarudishiwa baadae

8 Comments:

At 4:49 PM, Blogger luihamu said...

Mzee Ndabagoye afadhali hiyo,hapa mbongo nimeona nguzo ya umeme katika HIGHWAY sasa pata picha gari inagonga hiyo nguzo,hapatatosha.

Amani

 
At 6:06 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Egdio nimekutag.
Tujulishe vitu nane tusivyojua kuhusu wewe.

 
At 11:30 AM, Anonymous Anonymous said...

du bro unakaa mtaa wa kimasaki, aminia je watoto wa geti kali si matata sana mzee mtaa huo.aminia sana dizzle hapa

 
At 11:20 PM, Blogger Ndabuli said...

Naona utupe kwa Kamera ya maneno(kwa sababu walichukua kwa muda) mimi naipendelea sana

 
At 3:14 PM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Hivi Luihamu ile nguzo kama sikosei ipo Temeke kule,bado ipo tu?.Au kuna mizizi ya mababu pale?
Simon ile shughuli kweli ngoja nafanya mida f'lani mkuu.

Wanalindwa hawa kwa mitutu kaka.Hawachelewi kukutengua kiuno.
Ndabuli jamaa walichukua waliona nataka kuchukua picha za tukio kiaina wakajua soo kwa mkuu wao maana mama ndio alifanya soo lile.

 
At 6:13 PM, Anonymous Anonymous said...

Ndugu Egidio Ndabagoyey sijue wewe ndio kupiga picha ni kazi yako au upo kwenye hizi mtandao kama kujiosha, kwa my advice kama ndio pro yako ulikuwa unayoa haki ya kupiga picha, pili hapo wewe ndio unapoishi yaani nyumbani kwako so hapo sio ikulu au jeshini au police station ndio sehemu nyeti au muhimu kwa gov yoyote, kulikuwa hakuna police au mtu yoyote hangechukuwa camera yako kama unajua haki yako na ili ndio tatizo kubwa kwa bongo police, mtu mkubwa serikali au tajiri wanaweza kufanya kitu chochote ila watu or mtu kutetea haki yake na hii inatokana na wahandishi wetu wa habari, hawandikia au kuelimisha watu haki zao je mtu kama wewe ndio pro yako na haki yako unaogopa kufanya kazi yako je mtu wa kawaida itakuwaje .. kuna kitu kinaitwa human rite plz jaribu kuwaelimisha wananchini ili wajuwe haki zao pamoja na wewe ili kesho unapoona tokeo muhimu uwe na uhuru wa kufanya kazi yako free . plz kama tz kuna chama cha wahandishi wa habari na wanakaa kimya kwa mambo kama haya basi hatuna nchi hii ni 2007 yaani demokrasi world. thanx for put this text in you blog..

 
At 11:14 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Ndugu Anon kupiga picha ni kama kazi yangu napenda kupiga picha za matukio sio kwa minajili ya kuoata kipato lakini kama kumbukumbu zangu tu.

Kila sehemu viongozi kujiona Miungu watu ipo,wanatunga sheria kali ili kuwakandamiza watu wa tabaka la chini.Katika nchi hii watu wanaishi kwa matabaka toka enzi na enzi na wanasema hayawezi kuisha,tabaka la chini kamwe haliwezi kujichanganya na tabaka la juu,ni tofauti na nyumbani unaweza ishi popote pale lakini huku wale wa chini kuna "mitaa yao" kuna mitaa hawawezi fika na kama wakifika wataulizwa wanataka nini.Ni sawa na nyumbani kwa sasa tunapoelekea.

Kwanza fahamu kuwa hakuna demokrasia.Waandishi wa habari wanapoandika habari mhariri anazipitia na kutoa zile zinaweza kumuudhi "mkubwa" anaacha zile za "Rashid kagongwa na gari" nafikiri ni mfumo mbaya uliojengekana na kuna hili suala la rushwa.Unatoa kitu kidogo unaandikiwa habari unazotaka wewe ipo kila sehemu iyo.

 
At 8:39 PM, Anonymous Anonymous said...

Asante kwa jibu lakini swala lipo pale pale kama hukiwa mwandishi wa habari na pia unajua sheria sijue kama hata kuna kingozi hatakaweza kukuzuia ila tu ufuate sheria zote sawa na kama ujue sheria au haki yako ndio utapata haki maisha mwako. mfano kama police hakija nyumbani kwako kwa ajili ya kusearch anatakiwa hakiwa na search warrant pamoja na balozi na mashahidi na pia lazima hakuambia kuwa anataka kusearch kitu gani na kama una wakili unaweza kumzuia mpaka wakili wako wawe hapo kwenye tokea sasa kwa woga wetu vitu kama hivi unawahachia wafanya kama wanavyofanya hii ninakuambia kwa ajili wanahabari na wapiga picha ndio watakaoleta maendeleo so kwako wewe ulikuwa unawasiwasi wa kutopiga picha maana kwa ulikuwa nyumbani kwako , pili unayo haki yakupiga picha mahali popote ila tu sio sehemu vyeti.........

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

eXTReMe Tracker