Friday, July 03, 2009

Maskini wasichana wa kidosi!

Tangu nimefika udosini kilasiku lazima iwe ni kituko au ngeni kwangu,kuanzia kwa wanizungukao mpaka matendo yao.Mfano ukija kwenye suala la mahusiano wadosi sio kama sisi.Ni watu wa kujificha ficha sana matendo yao.Ni nadra sana kukuta jinsia mbili zikitembea barabarani na hata wakiwa utaona tu wanavyojaribu kuonyesha jamii kuwa sio wapenzi.

Naambiwa naa wenyewe ukiwa na rafiki yako wa kimapenzi huruhusiwi kumleta ndani kwenye nyumba uliopangisha,mwenye nyumba ana haki ya kukuitia polisi.Na sio ajabu kuwakuta wanamalizia shida zao bustanini na kwenye migahawa.

Mara nyingi nimekuwa nawauliza kwanini pamoja na kuwa waaminifu kwa wenzi wao na wasiooa kutoruhusiwa kuwa na wapenzi iweje maambukizo ya ukimwi yapo juu kuliko sehemu nyingine ambazo mambo ni mswano tu kama Bongo? sipati jibu la uhakika zaidi ya vijana kulaani mila zao kuwa zimepitwa na wakati.

Wanawake baadhi ya sehemu udosini wanachukuliwa kama miungu,ni wasafi,watakatifu machoni mwa wanaume.Kwa hiyo sio kama bongo unampigia mluzi mwanamke utakavyo.Niliwahi kujaribu kutesti zali kumpigia mluzi msichana mmoja polisi waliokuwa karibu walisogelea na maswali kibao,nikawambia kwetu ruksa na sioni tatizo kumuita msichana hadharani kwa staili ya mluzi.

Udosini msichana akikupa namba yake ya simu hataki wengine wajue na anakupa masharti ya saa ngapi umpigie simu,baada ya hapo simu wanachukua wazazi! Ukiwauliza kama wanapenda jinsi wanavyobanwa wengi wanasema hawapendi wanavyobanwa.Ndio maaan wanapopata nafasi basi huitumia ipasavyo.

Sasa nyakati hizi udosini wanawake nawaonea huruma.Kuhalarishwa mapenzi ya jinsia moja ni pigo jingine kwao.

Thursday, July 02, 2009

Ushoga na usagaji ruksa udosini.

Leo wameshinda wakisheherekea ushindi wao mahakamani na kupata ruksa kuendeleza vitendo vyao vya kifirauni.Bonyeza hapa jaji alivyo ichambua sheria na kuwapa ruhusa.Angalia na hapa

Bado nipo nipo!


Mishe mishe kibao,masaa hayatoshi kila siku bora ya jana.Tutafika tu.Hali ya hewa hii lazima nipite kwa mshikaji wangu kupunguza makali ya joto.

Ukimchunguza bata hutamla!

Saturday, June 13, 2009

Mafua ya nguruwe udosini;msitaharuki asema Waziri wa Afya

Wadosi ni watu wasiojali na wanaosahau mapema.Majanga udosini ni kawaida wanadai wamezoe, mshikaji mmoja wakati ule wa mashambulizi ya kigaidi Mumbai aliniiambia nisitaharuki sana mambo madogo haya yanakuja na kupita.Kula maisha.Baada ya kugundulika watu takribani 16 wameambukizwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe udosini Waziri wa afya kaja na mpya bonyeza hapa

Monday, March 30, 2009

Conficker mnyoo hatari aprili mosi

Aprili mosi inasadikiwa tarakishi zipatazo milioni 12 duniani kote zitaathirika kwa mnyoo uitwao Conficker .Kinachoogopesha zaidi ni kwamba kimnyoo hiki haijulikani hasa ni kitu gani kitafanya.Tarakishi iliyoathirika itatengeneza kile kinachoadikiwa tarakishi yenye uwezo mkubwa katika kufanya lolote baya kwenye tarakishi za watu bila kipingamizi chochote.

Tayari kampuni ya Microsoft wametoa bakshishi ya $ 250000 kwa yeyote atakaetoa taarifa na kukamatwa wahusika waliondika programu hii.Ni muhimu kujua jinsi ya kuweza kujikinga na mnyoo huu ambao moja ya madhara yake makubwa unafuta kazi zako na kuharibu mfumo mzima wa muingiliano,bonyeza hapa usome maelezo zaidi na jinsia ya kujikinga.

Sunday, March 22, 2009

Wanachuo wanahitajika One laptop per Child.

Ule mradi wa kutoa tarakishi za mapajani za bei chee za dola 100 One Laptop per Child unahitaji timu ya wanafunzi wa vyuo watakao zunguka nchi moja kati ya 53 za Africa kusambaza tarakishi za mapajani.Bonyeza hapa upate maelezo kamili.Kumbuka mwisho wa kuwasilisha makisio/proposal ni tarehe 27 mwezi huu.

Sunday, February 15, 2009

Virusi vya Valentine

Siku kama ya jana kuna watu ambao kwa namna nyingine wao ni kuharibu tarakishi za wengine na au kunyakua password.Nimepokea barua pepe na kadi pepe kibao zikinitakia siku ya wapendanao.Kitu ambacho nimekuwa nafanya ni kuzifuta,bila kuzisoma.Ukifungua tu imekula kwako.Bonyeza hapa some zaidi.

Nashauri kama ukipata barua pepe za namna hiyo kwa mtu usiomjua ama usifungue kabisa au ukifugua kuna link mule ndani usiifungue.Tuendelee kupendana

Unajua?

Nilikuwa sifahamu.Wewe ulikuwa unajua?soma hapa

Saturday, January 17, 2009

Tuchangamkie fursa Google

Hata kama bado upo chuoni unaweza kujaza kuna "intern" kwa ambao hawajamaliza shahada zao.Bofya hapa

eXTReMe Tracker